Pages

Subscribe:

Monday, February 19, 2018

OKWI WA BUKOBA AKABIDHIWA RASMI JEZI YAKE YA MSIMBAZI



Yule kijana shabiki kindaki ndaki wa mshambuliaji wa Simba SC na timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi, mkazi wa Bukoba leo amekabidhiwa rasmi jezi ya klabu hiyo yenye jina na namba la mchezaji huyo.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Adam Abubakary amekabidhiwa jezi hiyo kutoka kwa kiongozi wa mashabiki wa Simba mtandaoni anayefahamika kwa jina la...
J-Munyama wa Mabibo Dar es Salaam.


Kijana huyo ambaye ni shabiki wa Simba SC alijitokeza kwenye gari ya matangazo ya Azam TV katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba, Februari 11 mwaka huu wakati wa mchezo kati ya Kagera Sugar na Azam FC na kujitambulisha kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Simba SC.

0 comments:

Post a Comment