Pages

Subscribe:

Tuesday, December 27, 2016

CHRISTIAN BELLA: DIAMOND NI SUKARI ALIKIBA NI CHUMVI


Mkali wa masauti Christian Bella Obama amefunguka juu ya u-team ambao unaendelea kkkatika tasnia ya muziki hapa Tanzania especially Team Kiba na Team Diamond.

Akiongea na E-News ya EATV Christian Bella amefunguka kuwa hao wote ni wasanii wazuri na kila mmoja anafanya vizuri kwa upande wake kama ni mtu unaeelewa wala huwezi...
kuwafananisha.

“Lazima usifie watu wanapofanya vizuri, Simaanishi kwamba Diamond ananizidi mimi kwenye vocals na vitu vingine, no, lakini Diamond ni msanii ambaye anajituma sana halafu amefanye vitu ambavyo hakuna aliyetegemea kwamba Diamond atakuja kufanya hivyo, kwanini tusimpe heshima? Kumpongeza mtu aliyefanya vizuri, ukiwa unampongeza mtu aliyefanya vizuri hata na wewe utafanikiwa, tusiwe na roho mbaya.” Alisema Christian Bella.

Mkali huyo hitmaker wa ngoma ya Nishike alifunguka kuwa kwa mwaka huu wa 2016 anawapongeza wote wawili na kudai kuwa wawili hao ni kama Chumvi na SUkari.

“Alikiba na Diamond ni watu wawili tofauti, Diamond kafanya vitu vyake vizuri na pia Alikiba kafanya vitu vyake vizuri, huwezi kuwafananisha, ni kama Sukari na Chumvi, Sukari ina umuhimu wake na Chumvi pia ina umuhimu wake. Utaichukia chumvi kwakuwa ni chumvi lakini ikikosekana kwenye mboga huwezi kula chakula, sukari utasema kwamba ina kisukari lakini ukienda kunywa chai ni lazima uweke sukari. Ni vitu viwili tofauti na kila kitu kina umuhimu wake.” Aliongeza Christian Bella.

Christian Bella alimaliza kwa kuacha sintofahamu kwa kushindwa kuweka wazi kwa mashabiki kuwa kwa upande wake yeye nani ni sukari na nani ni chumvi.

0 comments:

Post a Comment