Pages

Subscribe:

Tuesday, December 13, 2016

B HITS YASITISHA KUSAJILI WASANII NA KUWARUDISHA WASANII HAWA


B Hits: Hatusajili Wasanii tena wala haitatokea kuwarudisha tena Wakina Mabeste, Vanessa, Jux, M Rap na wengine.
Uongozi wa studio ya Muziki yenye maskani yake Mbezi jijini Dar es Salaam B Hits, umedai kuwa hawana mpango wa kuwasajili Wasanii wengine ama kuwarudisha Wakina Mabeste, Vanessa Mdee, Jux, M Rap na wengine waliokuwa chini yao awali.

Akiongea kupitia kipindi cha Chipuka cha Times Fm, Mratibu wa B Hits Aman Joachim, amedai wamejifunza kutokana na Makosa kwani waliwekeza pesa nyingi kwa...
ajili ya Wasanii hao bila ‘Kuambulia’ Chochote.

“Hakuna Msanii ambaye alikuwa chini yetu zamani akarudi tena No way, wala hatuhitaji wasanii wengine, tuliwekeza bila kuingiza chochote yaani tunakuwa na jina kubwa lakini hatuna kitu mfukoni, hatufanyi tena hiyo biashara” Alisema Amani.
Katika hatua nyingine B hits imewataka Wasanii kupuuza taarifa za kwamba studio hiyo inatoza hela nyingi za ‘Production’ kitu ambacho si kweli kwani gharama zao ni za kawaida kabisa.

0 comments:

Post a Comment