Pages

Subscribe:

Friday, December 23, 2016

ICE BOY: YOUNG KILLER ANA ROHO MBAYA


14607148_209506012836579_1678805950393221120_nRapa Ice Boy ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Tumbua majipu’ amefunguka na kusema Rapa Young Killer alikuwa hapendi kuona yeye anafanikiwa na kutoka kwenye muziki licha ya kufanya naye kazi kama ‘Back vocal Artist’ kwa miaka mitatu.

Ice Boy alisema baada ya kugundua Young Killer anambania na kutotaka msanii atoke aliamua kuachana naye na kufanya mambo yake mwenyewe mpaka...
alipofanikiwa kutoka ngoma yake ya kwanza na kupokelewa na mashabiki.

“Ujue nilikuwa na miaka mitatu nafanya ‘back vocal’ kwa Young Killer, hivyo muziki wangu mimi nimeanzia kwake toka mwaka 2012 yaani toka wimbo wake wa kwanza mstari wa kwanza anaandika mimi nipo naye.” 

Aliendelea “Baada ya muda sana nikaona mchizi hanipi ‘support’, mchizi hataki mimi nitoke mwenyewe ile support kwamba ananikubali haikuwepo tena nikasema siyo kesi kama hanikubali ngoja nijikate zangu nifanye michongo yangu na mimi nifanye kazi zangu binafsi.  

Ile kitendo cha kutoka nahisi ndiyo akawa na jelous so akawa anakunja kabisa, mimi sikutaka kwenda kwenye ‘media’ sababu ingeniharibia msanii mchanga sina ngona hata moja halafu napenda kiki nikaona siyo kesi ngoja nihangaike nitoe kazi nzuri mashabiki watanipenda na nitapata tu mashabiki kama yeye alivyopata”. Alisema Ice Boy kwenye ‘Ngaz kwa Ngaz’

0 comments:

Post a Comment