Pages

Subscribe:

Saturday, December 31, 2016

HARMONIZE: WCB HAKUNA CHUKI WALA USHINDANI KATI YETU



Harmonize amedai kuwa hakuna ushindani ndani ya lebo ya WCB wala chuki tofauti na watu wengine wanavyodhania. Hitmaker huyo wa Matatizo, amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa ndani ya lebo yao hawajawahi kushindana wala wanapotoa nyimbo hawatoi kwa mashindano kati yao ila mashabiki ndio wanaowachukulia hivyo lakini kibiashara kwao inakuwa vizuri.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa hakuna msanii wa lebo hiyo anachukia pindi mwingine anapofanya kolabo na msanii mwingine mkubwa kwa kuwa kila mtu anakuwa...
na riziki yake na mafanikio ya mmoja ndio yakwao waote.

Pia Harmonize amesema kuwa si kweli kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuwa wanaachia nyimbo zao kwa ajili ya kuzizima nyimbo za wasanii wengine na kuda kuwa wao wamepeana muda na kila mtu ana muda wake waliopeana kuachia nyimbo zao.

0 comments:

Post a Comment