Pages

Subscribe:

Tuesday, December 27, 2016

MADEE AKASIRISHWA NA PICHA PAMOJA NA VIDEO ZA CHID BENZ


Baada ya kusambaa kwa picha na video tofauti tofauti za msanii Chidi Benz akiwa amerudi katika hali yake ya matatizo kama aliyokuwa nayo mwanzo, Madee ameonyeshwa kukerwa na kitendo cha watu ambacho wanafanya kwa msanii huyo mkongwe wa HipHop.

Kupitia kurasa yake ya Twitter, Madee ameandika ujumbe ambao unaonyesha kutopendezwa na picha zinazokuwa zinarekodiwa zikimwonyesha Chidi Benz, Madee amefunguka na kusema...
kwamba kufanya hivyo ni kuzidi kumdhalilisha? au mnataka Kiki?.
Jambo hili limewafanya mashabiki kuanza kutengeneza maswali mengi kwa Madee kwamba kwa kusema “Madee anatatizo na Solo Thang au”?, Maswali hayo ambayo wanajiuliza mashabiki yamekuja baada ya kuunganisha tukio la Rapper Solo Thang hivi karibuni kwa kuposti kipande cha video katika kurasa yake ya Instagram akiwa na Chid Benz huku akiandika ujumbe wa kusikitishwa na hali aliyokuwanayo Chidi.

“Met with my Young brother Chid Benz last night almost cried, I dont judge, no matter what still my hommie, tumeongea sana, tuzidi kumuombea Mola”

0 comments:

Post a Comment