Pages

Subscribe:

Thursday, December 29, 2016

CHEMICAL: NIMEKUWA SURPRISED BAADA YA KUPATA UJUMBE WA STEREO



Baada ya rapper Stereo Jumatano hii kutoa la moyoni kwa kueleza jinsi anavyompenda rapper Chemical, Chemical amefunguka na kuzungumza kauli hiyo huku akidai ni kitu ambacho hakukitegemea kusikikia kutoka kwa rapper huyo.

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumatano hii, Chemical amedai baada ya kumsikia Stereo redioni ni wazi inaonyesha anachokisema Stereo kinatoka moyoni mwake ila kwa sasa...
hawezi kuzungumza lolote kwani yeye anampenda Stereo kama kaka yake.

“Kiukweli nimekuwa surprised sana kumsikia Stereo sikutegemea kumsikia akizungumza maneno hayo ila anavyozungumza alikuwa akiongea kwa hisia inaonyesha jambo hilo linatoka moyoni mwake,” alisema Chemical
Hata hivyo mashabiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii wamekuwa wakimdhihaki rapper Stereo kwa kushindwa kumface Chemical na kwenda kwenye vyombo vya habari.

0 comments:

Post a Comment