Pages

Subscribe:

Tuesday, December 20, 2016

VANESSA MDEE APATA SHAVU LA UBALOZI


Hitmaker wa ngoma ya Cash Madame Vanessa Mdee leo hii ametusanua kupitia kurasa yake ya Instagram kuhusu shavu lake jipya ambalo amelipata la kuwa balozi wa Slimtea. Vanessa Mdee ameshindwa kabisa kuzificha hisia zake na kujikuta akiandika ni jinsi gani anajiskia baada ya kudondokewa na shavu hilo nono na kuona kuwa ni nafasi nyingine ya kuikuza brand yake.

“Ninafuraha sana ya kutangaza kwamba mimi ni balozi mpya wa @slimteaglobal ni hatua nyingine kwenye kukuza brand ya...
Vanessa Mdee. Asante @Mr_Phiny kwa kufanyikisha hii. Jinsi ya kupata chai yako hapa nchini Tanzania nitakufahamisha hivi punde pamoja na offer kibao za siku kuu.” Aliandika Vanessa Mdee.

screenshot-www.instagram.com-2016-12-19-11-27-14
Kila la kheri kwa Vanessa Mdee katika utendaji wake mwema wa kazi yake hiyo mpya ya Ubalozi.

0 comments:

Post a Comment