Pages

Subscribe:

Monday, December 19, 2016

DARASSA ATOA UJUMBE HUU KWA WADAU WA MUZIKI BAADA YA KUNUSURIKA KIFO


Issue ambayo ilitrend kuliko kwa siku ya jana ni kuhusu ajali ambayo aliipata hitmaker wa ngoma ya Muziki Darassa CMG akiwa na Hanscana, Mr VS pamoja na Abbah producer, wakiwa njiani kutoka Kahama kwenye show kuelekea Kakola ambako pia alikuwa anaelekea kwenye show.

Taarifa zilitufikia mapema baada ya ajali hiyo lakini hatukufanikiwa kumpata Darassa kwa wakati huo kutokana na taratibu za kisheria zilizokuwa zikiendelea pande hizo. Sasa leo hii mwandishi amefanikiwa kumkamata Darassa kwenye exclusive interview na ameweza kufunguka...
mengi ikiwa kikubwa ni kutoa shukrani kwa wote ambao walionyesha kujali baada ya kufikiwa na taarifa hizo.

“Brothers and sisters, ndugu zangu nipo sehemu inaitwa Kakola, na ilikuwa ni almost kufika hapa kabla ya kupata ajali. Ni kweli tumepata ajali mbaya ila nshukuru Mungu tuko poa. Sikupata nafasi ya kupokea simu wakati napigiwa kutokana na utaratibu uliokuwa ukiendelea, lakini nimeona missed calls na message za ndugu zangu wote, ahsanteni sana kwa ku-care, najua tuko pamoja sana.”

0 comments:

Post a Comment