Pages

Subscribe:

Tuesday, December 20, 2016

KILLY: NIMEJIPANGA ILI KUHAKIKISHA NAPIGA HATUA KIMUZIKI


Msanii wa muziki aliyewahi kufanya vizuri na wimbo, Rudi, Killy baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na hivi karibuni kuachia wimbo mpya ‘Nikwambie’, amedai wasanii wachanga wanakabiliwa na changamoto nyingi lakini yeye anamejipanga kukabiliana nazo ili kuhakikisha anapiga hatua katika muziki wake.

Akiongea wiki hii, Killy amedai wasanii wengi wachanga wanaingia kwenye game bila kujiandaa vizuri kwa kuwa na kazi nzuri ambazo...
zinaweza kuleta ushindani kwenye game.

“Mimi naamini kila msanii ana nafasi yake katika muziki kama akifanya kazi nzuri ambayo inaweza kuwashawishi mashabiki kuisikiliza,” alisema Killy. “Tatizo au changamoto ambayo tunayo wasanii wengi wachanga tunaandaa ngoma ambazo haziwezi kuleta ushindani kwenye game, sasa utawezaje kufanya vizuri. Kwahiyo mimi binafsi nilikaa kimya kidogo kuangalia wapi tunakoseaga na nimejitahidi kujipanga ili kurekebisha makosa,”

Muimbaji huyo ambaye yupo chini ya kampuni ya Al Jazeera Entertainment ya Papa Misifa, alidai msanii hata awe na bosi mwenye pesa kiasi gani kama hana mipango mizuri pamoja na kazi nzuri hawezi kwenda sehemu yoyote.
“Mimi namshukuru Mungu pamoja na team yangu, imejipanga kikamilifu, lakini kabla ya kujipanga tulianza kuandaa ngoma ambazo zitaleta ushindani,” alisema Killy.

0 comments:

Post a Comment