Pages

Subscribe:

Saturday, December 10, 2016

DIAMOND AWAKIMBIZA RIHANNA NA DRAKE HUKO YOUTUBE

Video ya wimbo wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Raymond, Salome, ndiyo video ya muziki iliyotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube nchini Kenya, kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, kupitia takwimu ilizozipata.

BBC Swahili wamedai kuwa kwenye orodha ya nyimbo 10 kutoka duniani kote, nyimbo za Tanzania zimetazamwa zaidi. Takwimu hizo zinadhihirisha jinsi ambavyo Wakenya wanapenda... muziki wa Bongo Flava kuliko nchi nyingine yoyote ukitoa Tanzania yenyewe.

Hadi sasa, Salome ina views zaidi milioni 9.8 kwenye mtandao wa Youtube.

Hii ni orodha kamili:

Salome – Diamond Platnumz na Raymond

Work – Rihanna na Drake

Bado – Diamond Platnumz na Harmonize

Sauti Sol – Unconditionally Bae, na Alikiba.

Work from Home – Ty Dolla Sign na Fifth Harmony

This is What You Came For – Calvin Harris

Kwetu – Raymond

Cheap Thrills – Sia na Sean Paul

Pillow Talk – Zayn

Ain’t Your Mama – Jennifer Lopez

0 comments:

Post a Comment