Pages

Subscribe:

Saturday, December 10, 2016

DIAMOND ALIPOTOKA MUZIKI WA BONGO ULIPANDA, BENDI UMESHUKA


bella
Mkali wa masauti Christian Bella amedai mafanikio ya wasanii wa muziki wa bongofleva katika muziki huo ndio kitu ambacho kimeufanya muziki wa bendi kushuka na kuonekana haufanyi vizuri.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Nishike’ amedai Diamond ni mmoja kati wasanii hao ambao walileta mapinduzi makubwa katika muziki wa bongofleva.
“Alipotoka Diamond Bongo fleva ilianza...
kurudi na muziki wa bendi zikaanza kulala,”

 Bella alikiambia kipindi cha ubaoni cha EFM. “Ilipofika 2010 mabadiliko yakaongezeka akina Alikiba wakaanza kurudi kina Dully Sykes pia,”
Pia amesema yeye ni mmoja kati ya wasanii wa muziki wa bendi ambao waliushtukia mchezo mapema na kuamua kufanya muziki ambao unawavutia watu wengi zaidi.

Muimbaji huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio kwenye muziki wa sasa, hivi karibuni amezindua studio yake mpya ya muziki iitwayo Kingdom Music.

0 comments:

Post a Comment