Pages

Subscribe:

Tuesday, December 13, 2016

FIFA YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MCHEZAJI WA MBAO FC

fifa
RAIS wa Shirikisho la Soka duniani (Fifa), Gianni Infantino ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kufuatia kifo cha ghafla cha mchezaji wa Mbao FC, Ismail Khalfan.

Khalifan alifariki dunia baada ya kuanguka uwanjani Desemba 4, mwaka huu katika Uwanja wa Kaitaba, Kagera wakati timu yake ya Mbao ikicheza na Mwadui katika mechi ya ligi ya vijana wenye umri chini ya miaka 20.

Infantino, katika salamu zake kwa Rais Malinzi, alianza kwa kusema: “Tafadhali pokea salamu zangu za rambirambi baada ya...
kusikia kifo cha mchezaji Ismail Mrisho Khalfan ambaye ni mchezaji mwenye umri wa chini ya miaka 20.
“Kwa niaba ya wajumbe wa kimataifa wa mpira wa miguu, sina budi kutuma salamu hizi kwa familia nzima ya mpira wa miguu duniani na familia ya Khalfan iliyopoteza mpendwa wao.”

Salaam za rambirambi za Infantino, zinakwenda sambamba na za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania, Nape Nnauye na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou ambao walitangulia kutuma hapo awali.
Timu hiyo ya Vijana wa Mbao, kama zilivyo timu nyingine saba za Ligi Kuu, ilikuwa Kituo cha Bukoba katika ambayo kwa msimu huu imefanyika kwa mara ya kwanza. Timu nyingine Nane zilikuwa kituo cha Dar es Salaam.

Khalifan aliyeanguka uwanjani dakika ya 74, alipata huduma ya kwanza uwanjani hapo kutoka kwa madaktari, lakini baadaye taarifa za kitabibu zilionyesha amefariki dunia.

Kamati ya Tiba ya TFF, bado inaendelea na uchunguzi wa kifo cha mchezaji huyo kabla ya kutoa taarifa kamili ya kitatibu kujua hasa chanzo hasa cha kifo cha mchezaji huyo. Marehemu alizikwa Desemba 5, mwaka huu jijini Mwanza.

0 comments:

Post a Comment