Pages

Subscribe:

Sunday, December 18, 2016

AZMA MPONDA NDIYO MSANII WA KWANZA WA HIPHOP TANZANIA KUFIKISHA VIEWS MIL 1 YOUTUBE


Ikiwa bado story inatrend kwenye social networks na kwingineko mtaani namna ambavyo muziki wa hip hop unatawala soko nchini Tanzania.

Tumezoea kuona wasanii wa kuimba imba wakipiga views wa kutosha kupitia video zao, kitu ambacho sio kawaida kwa msanii wa kurap kufikisha views 1million, lakini hivi karibuni tumeshuhudia kutoka kwa...
Darasa ambaye amefikisha views 1million views ndani ya wiki mbili kupitia video yake ya Muziki,mwanaFA hali kadharika kafikisha 1million views kupitia video ya Dume suruali.

Smashkilimanjaro inakusogezea msanii wa kwanza wa hip hop Tanzania kufikisha views milioni moja youtube.
Anaitwa Azma Mponda marufu kama A.Z.M.A,kupitia video yake ya Jinsi ya kumfikisha mpenzi, Azma amekua msanii wa kwanza wa hip hop kufikisha views milioni moja huku akifuatiwa na wasanii wengine kama Darasa na mwanaFA.

Jinsi ya kumfikisha mpenzi ni ngoma aliyompa shavu msanii Kita chini ya producer Kona Beats mwaka 2015, kichupa kilipigwa na BETRAM arts

Mwanamuziki na lecturer Kinye kutoka chuo cha st.Augustine kupitia mtandao wake wa instagram aliwahi kuandika “najua meanstream hawakupi kipaumbele lakini wewe (Azma) ni msanii wa kwanza kufikisha veiws milioni moja”


P the Mc ni msanii mwingine aliewahi kuongelea record hii ya Azma kwa kuwataka watanzania hasa waandishi wa habari kuzingatia ukweli kwa kufanya uchunguzi kabla ya kuandika habari.
Unaweza kuitazama video ya Azma jinsi ya kumfikisha mpenzi hapa:

Watch Here 

0 comments:

Post a Comment