Pages

Subscribe:

Saturday, December 31, 2016

YEMI ALADE KUHUSIKA KWENYE TUZO ZA GRAMMY


Wakati mashabiki wa muziki Afrika nzima wakiwa wanasuburia tuzo ya Grammy kutoka kwa Wizkid kupitia wimbo wa Drake wa “One Dance”, Yemi alade amepokea mwaliko wa kuhudhuria tuzo hizo.

Afrika inazidi kusonga mbele na kufanya vizuri kwenye sekta ya muziki kwa kuwakilishwa na wasanii kibao kutoka kila pande ya Afrika, Sasa msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade anayetamba na...
kibao chake cha “TumBum”, ameamua kushare na sisi mwaliko wake alioupata kwa ajili ya kuhudhuria tuzo za Grammy zinazotarajiwa kufanyika Mwakani February 12 siku ya jumapili.


Kupitia kurasa yake ya Twitter Yemi Alade ameshare picha inayoonyesha ni mwaliko wa kuhudhuria tuzo za Grammy.

0 comments:

Post a Comment