Pages

Subscribe:

Sunday, December 18, 2016

NAY WA MITEGO: NINA NYUMBA YA MILIONI 300 TABATA

Juzi kwenye XXL ya Clouds FM Nay wa Mitegoalikuwepo kutambulisha ngoma yake mpya ambayo ameipa jina la Sijiwezi, Ndipo alipokutana na story ya list ya wasanii 10 wa Bongo Fleva ambao wamefanikiwa kumaliza ujenzi wa nyumba zao na ikiwa mtonyo wa kijenga nyumba hizo umetokana na music.
 
Diamond Platnumz alikuwa ni mmoja kati ya wasanii waliopo kwenye list hiyo ambaye yeye inasemekana amenunua nyumba yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Million 300 huko...
nchini South Afrika.

Ndipo Nay wa Mitego alipoikamatia hiyo kwa juu na kudai kuwa mjengo ambao Diamond Platnumzameujenga South Africa, yeye ameujenga hapa hapa Bongo pande za Tabata. Akiwa na maana kuwa nyumba yake ambayo ameijenga Tabata ina thamani sawa na nyumba ya Diamond Platnumz ya huko South Africa (Mil 300).

0 comments:

Post a Comment