Pages

Subscribe:

Tuesday, December 20, 2016

GIVE IT TO ME YA BELLE 9 YAMPAGAWISHA KIKWETE


kikwete na Belle 9
Mbunge wa Chalinze na mdau mkubwa wa sanaa na michezo nchini Ridhiwani Kikwete ameshindwa kujizuia na kuweka wazi mahaba yake kwa ngoma mpya ya Belle 9 iliyo zinduliwa mwishoni mwa wiki ya ‘GIVE IT TO ME’.

Ridhiwani ambaye alikuwa ni miongoni mwa wadau walio hudhuria uzinduzi huo alizungumza na kusema kuwa anampongeza sana Belle 9 kwa hatua hiyo video ni kali sana na yeye kama mbunge na kijana huwa anapenda...
kushirikiana na vijana wenzake ili kuweza kukuza sanaa yetu.

“Niliona kwenye page yake ya instagram akiwa Afrika ya Kusini kwa ajili ya ku’shoot’ video yake na kuwasiliana naye kuwa akirudi tuonane na kweli aliporudi tulikaa tukaongea akaniomba sehemu pale nyumbani afanyie huo uzinduzi nikampatia ndiyo kama unavyoona “ Alisikika kwenye eNewz

Pia aliongeza kwa kusema kwamba kitu kikubwa ambacho kimemvutia sana katika video hiyo ni jinsi alivyo tembea na “beat” ya wimbo huo pamoja na ile sehemu jinsi anavyo jitoa kwa mpenzi wake.

0 comments:

Post a Comment