Pages

Subscribe:

Tuesday, December 27, 2016

TIMBULO: SIJUTII KABISA KUACHA UALIMU

Msanii Timbulo ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usisahau' amefunguka na kusema toka ameacha kufundisha na kuachana na fani yake ya ualimu na kukimbilia kwenye muziki hajawahi kujutia maamuzi hayo kwani muziki umekuwa ukimpa mafanikio makubwa zaidi.

Timbulo alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo ya EATV na kusema saizi hakuna kitu kingine anachofanya zaidi ya muziki na kila kitu unachomuona nacho au anachomiliki ni kutokana na...
kazi yake hiyo ya muziki.

"Kwa kiasi kikubwa nafanya muziki wenye faida, niliacha kazi ya ualimu na kufanya muziki hivyo sijutii kabisaa kuacha ualimu kwani toka nimeingia kwenye muziki sijawahi kufanya kazi nyingine na kila kitu unachoniona nacho sasa au nachomiliki sasa ni kutokana na kazi yangu ya muziki na kama ningeendelea kuwa mwalimu nisingekuwa namiliki vitu nilivyonavyo sasa" alisema Timbulo 

0 comments:

Post a Comment