Pages

Subscribe:

Thursday, December 29, 2016

NANDY KUTOSAHAU HAYA KWA MWAKA 2016


Katika kuelekea kuumaliza mwaka huu wa 2016 kila mmoja anakuwa na kumbukumbu ya mambo muhimu ambayo yamemtokea ndani ya mwaka hadi kufikia kuumaliza, haijalishi kama ni mazuri au mabaya, yote yanaweza kukaa kwenye kumbukumbu.

Mwanadada Nandy amepiga story na smashkilimanjaro na kutusanua ni mambo gani ambayo kwa upande wake hawezi kuyasahau kwa mwaka huu wa 2016.
Ni dhahiri kabisa kuwa mwaka huu umekuwa ni...
wa mafanikio zaidi kwa mwanadada Nandy kutokana na mengi ambayo amekuwa akifanya kwa mwaka huu yamekuwa mswano. 

Ikiwa ni pamoja na kuwa mmoja kati ya washindi wa shindano la Tecno own The Stage ambalo fainali zake zilifanyika huko nchini Nigeria.
“Cha kwanza ambacho siwezi kukisahau ni jinsi nilivyoshinda kwenda Nigeria kwenye audition za Tecno Own The Stage, na nilivyoshinda kama mshindi wa pili na nilivyopata zile hela, tuzo na simu, hicho ni cha kwanza ambacho sitaweza kukisahau.”

0 comments:

Post a Comment