Pages

Subscribe:

Tuesday, December 27, 2016

BILLNAS: MUZIKI WANGU SIYO BIG-G



Rapa Bill Nas anayefanya poa na wimbo wake 'Chafu pozi' amefunguka na kusema muziki wake si 'Bubble gum' bali muziki wake unaishi na kudumu kwenye ramani ya muziki tofauti na aina ya muziki ambao unafanywa na baadhi ya wasanii ambao haudumu kwenye ramani.

Bill Nas amesema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo na kusema ngoma zake zote alizotoa hata zikipigwa leo bado zinafanya vizuri licha ya...
kutoka muda mrefu ukilinganisha na kazi za watu wengine.

"Unajua muziki wangu si 'Bubble gum' mfano ngoma yangu 'Chafu pozi; imetoka toka mwezi wa nne lakini mpka sasa ikipigwa inafanya vizuri na watu watapenda kusikiliza na kama wapo kwanja basi wataruka sababu ni muziki unaodumu, kuna ngoma nyingi za wasanii wengine zimetoka baada ya 'Chafu pozi' lakini saizi hawezi kufanya kama ngoma yangu inavyofanya, hivyo muziki wangu si bigijii" alisema Bill Nas

0 comments:

Post a Comment