Pages

Subscribe:

Sunday, December 18, 2016

SHOLO MWAMBA AFUNGUKA CHANZO CHA UGOMVI WAKE NA MAN FONGO


Hakuna asiyefahamu kuwa kuna bifu zito baina ya wakali wawili wa muziki wa Singeli Man Fongo na Sholo Mwamba. Hitmaker wa ngoma ya Ghetto Sholo Mwamba ametusanua chanzo na sababu kubwa iliyofanya wawili hao kuwa katika ugomvi huo mzito. 

Sholo Mwamba amedai kuwa sababu kubwa ya kutofautiana na Man Fongo chanzo ni aliyekuwa bosi wao wote wawili ambaye ni G Maker. Akidaiwa kuwa alikuwa na upendeleo na msanii mmoja ambaye ni...
Man Fongo baada tu ya ngoma ya Hainaga Ushemeji kuhit, hivyo akaamini ni Man Fongo pekee ambaye anaweza kuwa na mafanikio makubwa.

Sholo Mwamba amefunguka hayo kwenye kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV hapo jana akihojiwa na Sakina Lyoka kwenye kipindi hicho.
Sholo alidai kuwa yeye hana chuki kabisa na mwenziye Man Fongo ila tu ni tofauti za kibiashara ndio zinafanya asiwe na maelewano mazuri na mshkaji wake huyo, na pia alidai kuwa hayuko tayari hata kidogo kumaliza bifu na Man Fongo kwasababu ya kuupeleka muziki wa Singeli mbele kupitia bifu hilo.

0 comments:

Post a Comment