Pages

Subscribe:

Sunday, October 29, 2017

NIKKI WA II: NITAKAPO KUWA RAIS HAPO BAADAE HAKUTAKUWA NA NENO WAHAMIAJI HARAMU


Kila mtu ana ndoto na malengo yake ktk maisha anayo ishi na uzuri wa ndoto kama ukiiwekea malengo huwa inakupa asilimia 50 kwa 50 maandalizi yakiwa mazuri basi unaweza kufankisha jambo unalo liota, Moja kati ya ndoto kubwa za Nikki wa II kutoka kundi la weusi ni kuja kuwa kiongozi hapo baadae.

Mara kadhaa nikki amekuwa akipost point ktk mitandao yake ya kijamii ambazo kwa mtu mwelewa akisoma na kutafakari hawezi kutoka patupu lazma ujengeke kwa kiasi fulani na sasa Nikki ameamua kuweka wazi mambo makuu 8 atakayo yafanya endapo atakuwa Rais hapo baadae.  Nitakapo kuwa Rais hapo baadaee inshalla
1. Kikaoo kikubwa cha serikali yangu sio baraza la mawaziri itakuwa...

mkutano mkuu wa kijiji/ mtaaa (kitaa kinaongea)

2. Kipimo cha maendeleo kitakuwa kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi, makusanyo, au shilingi.. . 


3. Mfumo wa elimu utajikita kupima "learning" yani kujifunza sio kupima ufaulu na ufeli

4. Vyama vyenye nguvu vitakavyo kuwa vina fanya mikutano na kuihoji serikali sio vyama vya siasa bali vyama vya wakulima, wafanyakazi, walimu, machinga, boda boda, madactari nk

5. Serikali itakuwa mdau namba moja kwenye uchumi na mwekezaji atakuwa mkulima, mfugaji, mchimbaji mdogo, wavuvi wadogo na wafanyabiashara wa wadogo

6. Ardhi, elimu, maji, afya havitakuwa bidhaa bali hifadhi ya jamii

7. Maisha bila maadili hayana mana kila mtoto lazima afundishwe kuwa na adabu, uaminifu, heshima, ujamii, upendo, bidiii na kujiamini

8. Mahusiano na mataifa ya Afrika, hakutakuwa na neno wahamiaji haramu, mwafrika hawezi kuwa haramu afrika ni nyumbani kwao

Maswali mtaniuliza wakati wa kampeni ukifika....(mgombea binafsi)

0 comments:

Post a Comment