Pages

Subscribe:

Tuesday, October 24, 2017

CHRISTIANO RONALDO AUNGANA NA ZIDANE PAMOJA NA RONALDO DE LIMA

Nyota wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo usiku wa jana amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa kiume duniani akimubwaga mpinzani wake Lionel Messi wa Barcelona. 

Katika tuzo hizo zilizofanyika jijini London Ronaldo ametwaa tuzo hiyo ambayo sasa inamfanya kuhama kundi la Lionel Messi na kuingia kwenye kundi la Ronaldo De Lima na Zinedine Zidane ambao...
wametwaa tuzo hiyo mara tatu kila mmoja.

Ronaldo ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo na kufikisha idadi ya tuzo tatu ambapo mara ya kwanza alitwaa mwaka 2008 akiwa Manchester United.

Mwaka 2009 FIFA iliungana na chama cha soka cha Ufaransa na kuunganisha tuzo hiyo ikafahamika kama Ballon d.or ambapo Messi aliitwaa kwa mara ya kwanza. Mwaka 2016 FIFA walivunja mkataba wao na Ballon d’or kisha kurejesha tuzo ya FIFA ambapo Ronaldo alitwaa pamoja na mwaka huu.

Naye Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amekuwa kocha bora wa soka la wanaume (BEST FIFA MEN’S COACH 2017) akiwagalagaza Massimiliano Allegri wa Juventus na Antonio Conte wa Chelsea.

0 comments:

Post a Comment