Pages

Subscribe:

Friday, October 27, 2017

NIKKI WA II: WAZO KAMA UMELIWAZA NA KUKAA NALO KICHWANI HAINA MAANA


Msanii wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameeleza sababu ya kupendelea kuandika mambo chanya (positive) katika mitandao ya kijamii.

Rapper huyo amesema kuwa anapendelea kufanya hivyo kutokana huwa anajifunza/kusoma vitu vingi hivyo kila ambacho anakuwa amekipata kwa wakati huo anaamua...
kuwashirikisha na wengine.

“Unajua wazo kama umeliwaza ukikaa nalo linakuwa halina maana, kwa hiyo ukishare uwezi kujua, mtu mwingine anaweza kuliendeleza kutokea pale, unaweza kumsaidia mtu kutazama kitu tofauti na alivyokuwa akitazama zamani” Nikki wa Pili ameiambia Bongo5.

“So all idea ya kuandika mambo katika Instagram ni kushare mawazo ili na mimi nipate feedback, kwa sababu unaweza ukawa umejifunza kitu inakuwa wewe ndio umejifunza vile huenda watu wengine wengi wanajua tofauti, so unapotoa mawazo yako unatoa nafasi ya kusikia mawazo mengine” ameongeza Nikki.

Nikki amekuwa akiandika mambo mbali mbali kama vile siasa, muziki, mahusiano, elimu, uchumi nakadhalika katika mitandao yake ya kijamii ya Instagram na twitter.

0 comments:

Post a Comment