Pages

Subscribe:

Saturday, October 28, 2017

CATALONIA YASHINDA KWENYE KURA ZA KUWA TAIFA HURU

Bunge la Catalonia limepiga kura ya kujitoa Spain, na kuibuka na ushindi wa kishindo kwa kupata kura 70 za wabunge waliokubali kujitoa, na kura 10 za wale waliopinga. 

Zoezi hilo la kupiga kura limefanyika leo, huku kukiwa na usiri mkubwa kwa wale waliopiga kura za kujitoa, baada ya Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo kuahidi kuwashtaki watakaopiga kura ya kukubali kujitoa, kwa kosa la...
uasi.

Waziri Mkuu wa Spain, Mariano hapo awali alisema utawala wa moja kwa moja ulikuwa unahitajika kwa nchi hiyo kwa sasa, ili kurudisha sheria, demokrasia na utulivu.

Mwanzoni mwa mwezi huu raia wa Catalonia walianza vurugu kudai uhuru kutoka kwa Spain, baada ya kuona wako tofauti na wao kitamaduni, lugha na pia kuwa na jeshi lao la polisi.

Maseneta wa Spain pia watatakiwa kupiga kura kwa mara ya kwanza kutekeleza kifungu cha sheria za Spain cha 155, ambacho kinaipa mamlaka serikali kuchukua hatua zote muhimu kulazimisha jimbo likiwa katika mgogoro

0 comments:

Post a Comment