Pages

Subscribe:

Sunday, October 22, 2017

BABA LULU: SIHITAJI POSA KWA ANAYEHITAJI KUMUOA LULU



Baba mzazi wa msanii wa filamu Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’, Mzee Kimemeta amefunguka mambo kadhaa kuhusu mwanaye kuolewa. 

Akizungumza na East Africa Radio, Mzee Kimemeta amesema kwanza hana shinikizo kwa mwanaye aolewe na mtu fulani kwa sababu ni maarufu bali ni maamuzi yake binafsi na suala la posa...
kwake halipo.

“Suala la kuoana mimi halinihusu ni suala la watu wawili, anayeoa na anayeolewa, yeyote atakayemleta akaniambia baba huyo ndio wangu sisi tunambariki” amesema.
“Hapa, sisi kwa kweli posa haipo katika msamiati wangu, siuzi mtoto wala sitaki posa yoyote, posa yangu ni amani ndani ya nyumba yao, ndio posa watakayoniletea,” amemaliza kwa kusema.

0 comments:

Post a Comment