Pages

Subscribe:

Thursday, October 26, 2017

HATMA YA ELIZABETH MICHAEL (LULU) KUJULIKANA NOVEMBA


A @laviemakeup Beat...!!!!💚💚💚
#szifflaunching 
#hakikanizakwetu

Kesi inayomkabili Elizabeth Michael ambaye ni muigizaji wa filamu bongo ya kuua bila kukusudia, inatarajiwa kufikia hatma yake baada ya Mahakama kusema kuwa hukumu itatolewa Novemba 13, 2017. 
Kesi hiyo ambayo imesikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, imesema imemkuta Elizabeth Michael na hatia ya kumuua bila kukusudia muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake, baada ya kusikiliza maoni ya...
Baraza la Wazee hii Leo.

Wazee hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.

Kabla ya  wazee kutoa maoni, Jaji Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni hayo ya Baraza la Wazee.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 13, ambapo hukumu yake itasomwa.

0 comments:

Post a Comment