Pages

Subscribe:

Friday, October 20, 2017

PRODUCER WA FILAMU HOLLYWOOD AMTAKA LUPITA NYONGO KINGONO

Muigizaji wa Hollywood kutoka Kenya, Lupita Nyong'o, amesimulia jinsi producer mkubwa wa filamu wa Hollywood Harvey Weinstein alivyomtaka kingono wakati akiwa kwenye shule ya filamu akimuahidi kumsaidia zaidi. 

Akifanya mahojiano na moja ya vyombo vya habari vya New York nchini Marekani, Lupita ambaye ni mshndi wa tuzo ya Oscar alisema alikutana na producer huyo...
mwaka 2011 kwenye tamasha la filamu na kumualika nyumbani kwake, kwenda kutazama filamu mpya aliyotengeneza.

Akiwa nyumbani kwake na watoto wake wadogo baada ya dakika 15 kupita alimuita sehemu nyingine ya nyumba na kumpeleka chumbani kwake na kumtaka amkande mwili.

“Harvey alinipeleka chumbani kwake, akataka nimkande mwili, kwanza nilidhani anatania , nikajihisi sipo salama, nilihamaki kidogo na nikafikiria kwa haraka kumkanda ili nipate muda wa kufikiria jambo la kufanya, wakati namkanda akataka kutoa nguo zake nikamwambia hapana, sitajisikia vizuri kufanya hivyo”, alisikika Lupita.

Lupita aliendelea kusimulia kuwa...”Aliendelea kwa kunialika tena kutazama filamu (screening) New York na nilienda kuungana naye, nilipofika kule kumbe alikuwa peke yake, na moja kwa moja akaenda kwenye point akisema kuna chumba juu cha kupumzika kwa muda wa chakula, nikamwambia ni bora tupate chakula mgahawani, akaniambia nisiwe mjinga, kama nataka kuwa muigizaji niwe tayari kufanya vitu kama hivi na kunaimbia ameshatoka na wanawake wengi wa Hollywood na alipowafikisha”.

Lupita sio msanii wa kwanza kulalamikia suala la kuombwa ngono na producer huyo ili amfanye kuwa maarufu, kwani wasanii wengine wa kike wameshalalamikia vitendo vya producer huyo ambaye ameshatengeneza filamu kama 'Shake Spear in love' na 'New York Gang'.

Wiki iliyopita Polisi jijini New York walianza uchunguzi dhidi ya producer huyo ambaye amehusishwa na vitendo vya ubakaji.
 
Producer Harvey Weinstein

0 comments:

Post a Comment