Pages

Subscribe:

Monday, October 30, 2017

WASANII WA MUZIKI NCHINI KENYA WABEBESHANA ZIGO LA LAWAMA

Baadhi ya wasanii nchini Kenya wameanza kutupiana lawama kwa kukaa kimya bila kupaza sauti kwamatukio mya mauaji ya kisiasa yanaoendelea nchini humo. 

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Octopizzo ambaye hivi karibuni alimvaa msanii mwenzake Jaguar akimtuhumu kukaa kimya bila kuchukua hatua yoyote juu ya vijana wa eneo lake wanaofanya vurugu hadi...
kufikia hatua ya kuuana, kutokana na migogoro ya klisiasa inayoendelea.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Octopizzo ameandika ujumbe ukienda kwa wasanii wengine akisema  
"Wale wasanii wote wamenyamaza badala ya kukemea mauaji na manyanyaso ya Mban’ga Kawangware, Odhumo,Bungoma na mitaa mingine kadhaa, mashabiki na watoto wasio na hatia wanauliwa na hamuongei alafu mnatutolea ngoma za kifala mkidai support na kura za mashabiki, tunawaona na tunawangoja sana, simama kwa ajili ya watu hata kama ulikula pesa ya kampeni, jaribu kuvaa viatu vya wale watu ambao wamepoteza watoto wao wasio na hatia, hizo ngoma zenu mtazisikia studio tu sasa hivi, unajiiaje msanii kama huwezi kuwawakilisha wale wanaokuangalia?”.

Kitendo cha mauaji yanayoendelea nchini Kenya, kimefanya baadhi ya wasanii Kenya kutoa nyimbo zikilaumu kwa nini hali hiyo inatokea, akiwemo Nameless ambaye ameachia wimbo unaoitwa 'Ooh Why' unaozungumzia hali ya machafuko yaliyosababishwa na siasa.

Hali ya usalama nchini Kenya hivi sasa imekuwa si nzuri kutokana na vurugu zinazoendelea, na kusababisha vifo vya watu mbali mbali wakiwemo watoto wadogo wasio na hatia.

Alichokiandika Octopizzo

0 comments:

Post a Comment