Pages

Subscribe:

Friday, October 27, 2017

MAPACHA WALIOSHIKANA VICHWA WAFANIKIWA KUTENGANISHWA


madaktari wa upasuaji katika mji wa India Delhi wamefanikiwa kutenganisha  wavulana pacha waliokuwa wameshikana kichwani, wavulana hao wa miaka miwili (jaga na kalia) walifanyiwa upasuaji uliochukua takribani saa 16 na sasa wako katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, kulingana na taarifa za madaktari.
 
kundi la madaktari 30 walifanya upasuaji huo katika taasisi ya matibabu ya sayansi  ya All India. wavualana hao walizaliwa wakiwa wanatumia...
pamoja mishipa ya ya damu mbali na tishu za ubongo, hali isiyo ya kawaida ambayo hutokea mara moja kati ya watoto milioni 3 wanaozaliwa

Mkurugenzi wa hospitali hiyo Randeep Guleria aliambia vyombo vya habari vya India kwamba siku 18 zijazo zitakuwa muhimu ili kuthibitisha ufanisi wa uchunguzi huo.
pacha hao wanaotoka katika kijiji cha mashariki cha jimbo la Orissa walikuwa wameshikana katika kichwa, hali inayoitwa ‘craniopagus’

0 comments:

Post a Comment