Pages

Subscribe:

Wednesday, October 19, 2016

Z ANTO APIGA CHINI OFA YA KUJIUNGA NA LEBO YA WCB

Muimbaji wa ‘Binti kiziwi’ Z-anto yupo tayari kurudi kwenye label iliyokuwa inasimamia kazi zake zamani, TipTop Connection. Mkali huyo aliyewahi kutamba zamani amesema pia kuwa alipiga chini dili la kujiunga na label ya WCB inayomilikiwa na Diamond kwa kile anachoamini kuwa mafahari wawili hawawezi kukaa zizi moja.
 
“Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka saizi kuna ‘label’ nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na...
moja kati ya hizo. Maana nikibugi kuchagua ‘label’ ambayo inaweza kunisimamisha kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. 

Nilikuwa na maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip Top Connection” Z Anto alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.
Z anto pia alifunguka kuwa sasa hivi yupo kwenye mazungumzo na label kubwa.

0 comments:

Post a Comment