Pages

Subscribe:

Sunday, November 27, 2016

JOH MAKINI: TUZO ZA EATV NI BARAKA KWANGU


 
Rapa mkali katika tasnia ya Bongo Fleva Joh Makini, amemwaga furaha yake ya kuwa miongoni mwa wasanii walioingia katika vita ya kuwania tuzo za EATV 2016 kupitia ngoma yake ya Don Bother na kusema kuwa kwake hiyo ni baraka. 

Ngoma hiyo imemuigiza Joh katika tuzo hizo kupitia vipenge viwili ambavyo ni Wimbo Bora wa Mwaka na Video Bora ya Mwaka. Katika katika kipindi cha FNL cha EATV, Mwamba wa Kaskazini amesema  amejisikia furaha na faraja kwa kiasi kikubwa kuona kazi yake inathaminiwa na...
kuingizwa katika tuzo hizo kubwa za muziki na filamu Afrika Mashariki, huku akiimwagia sifa EATV kwa kuthamini muziki wa Tanzania na kuanzisha tuzo hizo.

Pia, Joh a.k.a Mwamba wa Kaskazini hakusita kuufagilia muziki wa hip hop nchini Tanzania kwa kusema kuwa muziki huo ndiyo wenye nguvu zaidi kwa kuwa wasanii wake wengi ni wabunifu.

"Muziki wa hip hop kuingia kwenye category za tuzo hizi  ni sawa na kuipa hip hop heshima, tena ilitakiwa nyimbo za hiphop ziwe kwenye kila category" amesema Joh.
Akizungumzia mabadiliko ya aina ya muziki anaofanya kwa sasa, amesema hip hop inabadilika, na kwamba kwa sasa mwana hip hop yoyote akitaka kubamba na kuingia kwenye tuzo kama hizi anapaswa kuchanganya ladha kama alivyofanya kwenye Don Bother na Perfect Combo.

Akitoboa siri ya ngoma zake kufanya vizuri, amesema hakuna siri bali ni ubunifu, video kali na 'idea' zisizojirudia.

Kumpigia kura Joh Makini pamoja na wasanii wengine unaowakubali ingia hapa:- http://www.eatv.tv/awards

0 comments:

Post a Comment