Pages

Subscribe:

Tuesday, November 29, 2016

YOUNG KILLER: HAKUNA MSANII WA HIPHOP ANAYE LIPWA MIL 10 KWA SHOW

Young Killer
Msanii wa muziki wa hip hop nchini, Young Killer Msodoki amedai kuwa hali ya uchumi kwa wasanii wengi wa hip hop ni duni huku akidai hakuna msanii wa hip hop anayelipwa zaidi ya milioni 10 kwa show moja.

Rapa huyo alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV kuwa wasanii wa hip hop wanashindwa kutambiana kwa pesa kama wasanii wengine kutokana wengi wao kuingiza kiwango sawa cha pesa, Pia Killer amesema muziki wa sasa una changamoto nyingi na ili upate nafasi ni lazima...
uzungumziwe hivyo haoni tatizo la Young D kutupiwa dongo na Stamina kuwa hata mapaka kwa sasa wana’rap’.

Killer pia amesema anajipanga kurudi na kurekebisha kila kitu ambacho hakipo sawa.

0 comments:

Post a Comment