Pages

Subscribe:

Saturday, November 26, 2016

BEN POL: SIJAWAHI KUFURAHIA KUFANYA VIDEO KAMA ILIVYO KUWA KWA MUZIKI YA DARASSA


15056795_322345568149424_1416941223125450752_n
Kama umeitazama video ya wimbo mpya wa Darassa ‘Muziki’ aliomshirikisha Ben Pol, utakuwa umeona jinsi wanavyokula bata kiasi cha kukufanya uyatamani maisha yale.  Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa kinachoonekana ndicho kilichofanyika – walikuwa na muda mzuri kiasi cha kumfanya akiri kuwa hajawahi kufurahia kufanya video kama ilivyokuwa kwenye hiyo.

“Ni video ambayo nimefanya bila kuchoka. Kwasababu kwanza tulikuwa tunahave fun wamekuja akina Jux pale. Wale warembo pia waliwekuwepo, watu wako...
charming, wako very happ yaani,” anasema muimbaji huyo.

“Hata walinzi waliokuwepo pale pembeni walikuwa kama wanatutamani fulani, yaani tulikuwa kama tunahave fun kiukweli.”
Ben pia anasema aligundua kuwa Darassa ni mtu anayependwa na ni rahisi mtu yeyote kumzoea. “Naweza kusema Darassa ni mtu rahisi kufanya naye kazi.”

0 comments:

Post a Comment