Pages

Subscribe:

Thursday, November 24, 2016

MATONYA AWATAJA WASANII WAKE WALIOFANYA VIZURI MWAKA HUU


matonya
Matonya amewataja wasanii ambao kwa upande wake anaona wamefanya vizuri kwenye muziki kwa mwaka huu. Hitmaker huyo wa ‘Sugua Benchi’ amemtajia mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez majina ya wasanii hao huku wasanii wa kiume wakiwa wawili na wa kike wawili pia.

“Kwa upande wangu wasanii wengi wamefanya vizuri, kuna Raymond amefanya vizuri, Harmonize, amefanya msichana anaitwa, kuna huyu rapper wa kike anaitwa Chemical. Bongo tuna vichwa kiukweli kuna...
watu wengi,” amesema Matonya.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa wapo baadhi ya wasanii wanaoenda nje kushoot video kwa ajili ya kupanua wigo wa muziki wa Bongo Fleva lakini wengine huenda huko kwa ajili ya kufuata mkumbo kwani hata yeye akiamua kwenda kushoot video Somalia kuna wasanii watakaomfuata huko.

0 comments:

Post a Comment