Pages

Subscribe:

Saturday, November 26, 2016

KAULI YA MADEE KUHUSU BABU TALE KUMGANDA DIAMOND

Instagram photo by Madee Seneda_BL0AVzLjX0E - JPG
Msanii Madee ambaye ni miongoni mwa wasanii viongozi wa Tip Top conection inayo simamiwa na Babu Tale, amejibu tuhuma za meneja wao huyo kuitelekeza Tip Top na kuegemea zaidi kwa Diamond Platnumz.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema hawezi kupinga maneno yaliyopo mtaani kwani ni kitu kinacho onekana kwao, lakini ukweli ni kwamba Babu Tale hajaitelekeza Tip Top, isipokuwa Diamond amekuwa...
na projects nyingi zinazo hitaji uwepo wake kama meneja.

Hivi karibuni mashabiki wameibua hoja kuwa Babu Tale ameipotezea Tip Top na “kugandana” na Diamond, kwa sababu anafanya vizuri na safari za nje hazimuishi, kauli ambayo hata Niki Mbishi ameiimba kwenye wimbo wake wa Babu Talent.

0 comments:

Post a Comment