Pages

Subscribe:

Tuesday, November 29, 2016

MWANA FA: DUME SURUALI NI DARASA KWA VIJANA WA KIDIGITALI

MWANA-FA-12
Wimbo wa Dume Suruali ndiyo inawezekana ukawa msemo kwa Watanzania wengi kwa kipindi cha miezi kadhaa ijayo, hiyo ni kutokana na mashairi yaliyoandikwa na mtunzi wa wimbo huo, Mwana FA akimshirikisha V-Money.

Unazungumzia mwanaume anavyolalamika kulazimishwa kuhonga fedha kwa mwanamke. Mwan FA ambaye jina lake halisi ni bwana Hamisi Mwinjuma, amezungumza na kufafanua kile alichokiandika...
kwenye wimbo huo aliomshirikisha bi Vanessa Mdee.

Lengo lako hasa ni nini?
Ni kuwataka watu wasiwe wajinga kwa kuwa mapenzi ni hisia na siyo biashara. Matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara nyingi tu katika kizazi cha sasa. Sina maana ya kuwasema vibaya wanawake lakini tukumbuke hata upande wetu sisi wanaume kuna Malioo ambao wao wanapenda kuhongwa na wanawake, ujumbe huu ni maalum kwa pande zote.

Kwa nini Vanessa?
Vanessa ni aina ya wanawake ambao sisi wanaume tukimuona tunahisi ili umpate ni lazima umuhonge sana, sababu ya kumchagua yeye ni kwa kuwa anawakilisha vizuri wasichana wa aina hiyo ambao wengi wamekuwa na mitazamo hiyo.

Umetunga kwa kuwa yamekutokea?
Mimi ni msanii, nawakilisha mengi yanayotokea kwenye jamii, yapo yaliyonitokea na mengine watu wangu wa karibu na jamii kwa jumla, kuna vitu ambavyo unaongeza ili sanaa ikamilike lakini kwa ufupi nimezungumza ukweli.

Utunzi wa wimbo ulikuwaje?
Niliutunga ndani ya muda wa siku moja niliyoenda studio lakini ilinichukua mwezi mzima kuwa naurekebisha hapa na pale. Hata Vanessa nilipomweleza alikubaliana na wazo langu na kuamini utafanya vizuri.

Kwa nini ulichagua MJ Records?
Prodyuza wa wimbo huo ni Daxo Chali ambaye ni mdogo wake Marco Chali. Nilienda MJ kwa Marco nikamueleza nataka kazi fulani akanipa ‘beat’ mbili, nikachagua yangu na Vanessa naye akachagua hii ambayo ndiyo imetumika kwenye wimbo.
Tuliamua kuchagua hiyo kwa kuwa Vanessa alinishauri ni beat laini ambayo kwanza itakuwa na ladha tofauti ndiyo maana tukaitumia.

Umemtaja tajiri Salah kwenye wimbo, ni nani?
Huyu ni rafiki yangu wa karibu, ni mmoja wa watu wangu ambaye amekuwa anashangaa sana jinsi wanaume wanavyohonga.

0 comments:

Post a Comment