Pages

Subscribe:

Sunday, November 27, 2016

M-RAP AFUNGUKA SABABU YA KUBADILI STAILI YA KUCHANA


Rapa M-Rap anayetikisa kwenye uga wa Bongo Fleva na ngoma yake mpya aliyoibatiza jina la 'It is not too late' amefunguka sababu za kubadili mtindo wake wa kuchana katika ngoma hiyo, na kusema kuwa amebadilika ili kufuata soko la muziki huo kwa sasa. 

M-Rap ambaye amezoeleka kama rapa zaidi kwa kutengeneza ngoma za kuchana zaidi akifananishwa na ma'rapa' wengine wanaoendana kiumri kama vile Young D na Young Killer, katika ngoma hii mpya ameamua...
kuchanganya ladha na kuweka mitindo ya kuimba, huku yeye mwenyewe akiwa na 'flow' tofauti.

Akiitambulisha video ya ngoma hiyo kwa mara ya kwanza kupitia FNL ya EATV, Rapa huyo amesema muziki wa hip hop kwa sasa umebadilika, na ili msanii atoke, ni lazima abadilike kwa kuchanganya ladha tofauti huku akimtolea mfano Dogo Janja ambaye naye ameamua kubadilika katika siku za karibuni.

Amesema anaamini ngoma hiyo itakubalika kwa mashabiki na kwamba hawezi kupoteza mashabiki kwa sasa bali mashabiki wake wataongezeka kwa kuwa anawapa kitu wanachokipenda.

0 comments:

Post a Comment