Pages

Subscribe:

Saturday, November 26, 2016

YOUNG KILLER: MAFANIKIO NDIYO CHANZO CHA BIFU ZA WASANII


Sauti za bifu za wasanii wahiphop ni ndogo sana kuziskia ila kwa upande wa ndugu zetu wakuimba yaani ni full base.

Msodoki ameamua kuweka wazi ishu hii ya wasanii wa bongo kuwa na mabifu na kusema kwamba wasanii wengi wa bongo wa HipHop wanakuwa hawana mabifu kutokana wote kukosa...
mafanikio.

Akiongea na kipindi cha E-Newz ya EATV, Young killer aliamua kuwapa ukweli mashabiki zake kuwa mafanikio ni chanzo cha watu kuwa na mabifu,  kwahiyo ukija kwa upande wa wasanii wa HipHop inakuwa ngumu kuchukiana kwasababu ni wachache wenye mafanikio.

“Mimi naweza kusema, ujue bifu zinatengenezwa kwa mafanikio, ni wachache sana wasanii wa bongo wa hip hop ambao wamefanikiwa, kwa hiyo inakuwa ngumu hata kuchukiana, tunaoneshana tu chuki ile kwenye mitandao kuwekana sawa, lakini sio ile real bifu kama wenzetu. Wenzetu wa kuimba wana mafanikio, show Milioni 10, unaona mwenzako anapata zile lazima umaindi, lakini show za Milioni tatu tatu, mbili mbili zinawafanya hata wasiwe na bifu, wasichukiane. Lakini chuki zinakuwepo moyoni.” Alisema Young Killer.

0 comments:

Post a Comment