Pages

Subscribe:

Tuesday, November 29, 2016

YOUNG DEE AFUNGUKA UKWELI KUWA AMERUDIANA NA TUNDA

Ni kwamba habari ya mjini kwa sasa ni story kuhusu uhusiano wa kimapenzi uliokuwepo kati ya rapa Young Dee ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na Video Queen Tunda waliyeacha baada ya kutoelewana kupelekana polisi.

Baada ya kuwepo taarifa kwamba Tunda ameachwa na mwanaume anayetajwa kuwa alikuwa akimgharamia kwa kila kitu ikiwemo kulipia nyumba, kununua magari na starehe zote alizokuwa akizifanya kila siku, ikaja kuonekana ameanza kuwa...
karibu tena na Young Dee.

Leo Soudy Brown amepiga stroy na Young Dee ambaye ameeleza kuwa yeye na Tunda wako vilevile kama mwanzo hawakuwahi kugombana na ameamua kumsamehe Tunda kwasababu itakuwa kosa kubwa endapo hatamsaheme wakati yeye pia ana makosa makubwa zaidi ya hayo ya Tunda.

“Mimi nilikuwa na matatizo yangu mengi sana hata kufika hapa tu nimesamehewa sana vitu vingi katika watu ambao hawakutakiwa kusamehewa ni mimi ndio mana nimeamua kumsamehe, kwa yote ambayo Mungu amenisamehe nisiposamehe nitakua nakosea sana” – Young Dee

0 comments:

Post a Comment