Pages

Subscribe:

Thursday, November 24, 2016

CHUKI ZA WASANII ZAMUUMIZA KICHWA BARAKA DA PRINCE

barakahtheprince_-20160916-0002
Msanii wa muziki Baraka the Prince ambaye kwa sasa yupo chini ya label ya Rock Star 400, ameonesha kuumizwa na kutofurahi shwa na chuki za wasanii zinazo endelea kwenye game ya muziki wa bongo fleva.

Kwenye ukurasa wake wa Instagrama Baraka
ameandika ujumbe huku akiomba Mungu chuki hizo ambazo sasa zinazidi kuonekana wazi wazi ziishe.
Amesema chuki hizo ambazo zimeonekana kukuzwa sana na team za mashabiki, huku akilalamika kuwa zinachangia...
kuua game ya muziki wa bongo fleva.
 
“Mungu saidia game ya Tanzania tupendane na tuheshimiane(….) ina sikitisha sana team team zinarudisha sana music industry yetu nyuma.. tumekosa tunzo nyingi kubwa na za maana, sababu ya kukosa umoja na mshikamano wa mashabiki.. tuna tengeneza matabaka baina ya mashabiki na mashabiki… Heee Mwenyezi MUNGU ingilia kati swala hili”, aliandika Baraka kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hivi sasa wasanii wengi wamekuwa wakisema hakuna chuki miongoni mwao pale zina po kuwepo tetesi, na kusema kuwa mashabiki ndiyo wanaokuza chuki hizo kupitia team zao, jambo ambalo kila siku limekuwa ni tatizo kwenye game.

0 comments:

Post a Comment