Pages

Subscribe:

Wednesday, November 30, 2016

IZZO B: SIJAWAHI KUFIKIRIA KUACHA MUZIKI

14134660_223993528022914_2191708896182140928_n
Msanii wa hip pop, nchini, Emanuel Simwinga ‘Izzo Bizness’ ameweka wazi kwamba, hafikirii kuacha muziki hata atakapozeeka, kwa kuwa ndiyo maisha yake kwa sasa.

Izzo B aliliambia MTANZANIA kwamba, muziki ndio unaofanya maisha yake yawe alivyo sasa, hivyo hawezi kuacha muziki kwa kuwa ana historia nao na anauheshimu na...
ataendelea kuuheshimu hadi mwisho wa maisha yake.

“Naamini kwa kujituma zaidi kunaniongezea mashabiki wengi, naufurahia muziki wangu na napenda mashabiki wangu waendelee kuufurahia, hivyo nitajitahidi kuendelea kuwafurahia hadi nifikie mwisho wa maisha yangu,’’ alieleza Izzo B.

Izzo B kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Dangerous Boy,’ kupitia kundi lao la ‘The Amaizing’, ambao wapo mbioni kuachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Milele’.

0 comments:

Post a Comment