Pages

Subscribe:

Saturday, November 26, 2016

SHILOLE ARUDI KWENYE KAZI YAKE YA MAMA NTILIE

Instagram photo by Shishi bybee _she roll it_BNOdE - JPG
Hitmaker wa ngoma ya “Say my Name” Shilole ameamua kutazama upande wa pili wa biashara tofauti na muziki ikiwa ni katika suala zima la kujitafutia kipato.
Ikiwa muziki ni biashara ambayo inakwenda na wakati, mkali huyo ameamua kuitazama kwa jicho hilo ili kujiwekea misingi mizuri katika kujipatia kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Sio mara ya kwanza kwa Shilole kufanya biashara ya kuuza chakula, lakini kwa time hii ameamua kufunga kibwebwe na kuahidi kupambana na...
vikwazo vyote ambavyo alikutana navyo hapo awali na kujikuta kufeli katika biashara yake.

Akiongea na Shilole amefunguka kuwa kwasasa biashara hiyo ameamua kuiweka nyumbani kwake na kuona kuwa kuna urahisi na ulinzi zaidi katika suala zima la ulinzi wa mali zake na vitu kama hivyo.

“Napika mwenyewe, kwasasa nafanyia hapa hapa nyumbani. Mwanzoni nilifunga kwasababu waliniibia vifaa vyangu muhimu katika kazi, sema sasa hivi hamna noma kwasababu nipo nyumbani hapa hapa kuna security kwahiyo mwizi akija tu ananaswa na umeme” Alisema Shilole
Nataka nikupe nafasi ya kumsikiliza Shilole akiwa anamkaribisha mteja, ile kimama ntilie zaidi. Play hii video hapa chini kusikiliza akipiga story zaidi kuhusu kazi yake hiyo mpya.

0 comments:

Post a Comment