Pages

Subscribe:

Thursday, November 24, 2016

HII NDIYO KAULI YA DIAMOND KWA WANAO TAFUTA KIKI KUPITIA YEYE

Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wanaojua utamu wa kazi ya mziki wa bongo flava na faida aliyoipata tangu aingie katika tasnia hiyo iliyompa heshima kubwa hasa hapa bongo.

Jana mshale ya mchana kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Diamond amewachana wasanii wanaojaribu kutafuta kiki kupitia jina lake na sio kwa mambo mengine yenye...
faida zaidi kwenye kazi.

"Mimi nadhani watu wafanye kile ambacho wanaamini ili kufanikisha malengo yao bila kupitia mgongo wa mtu na kuendelea kwenye maendeleo yao tu, mi bora mtu aniambie ili nijue namsaidia nini tofauti ya kutumia jina langu kwenye mambo yake na hili lipo sana kwa baadhi ya wasanii wenzangu ,akijihisi tu anaanza kupotea kwenye game anatumia jina la mtu maarufu kama mimi." alisema Simba wa bongo.

0 comments:

Post a Comment