Pages

Subscribe:

Monday, November 28, 2016

SHAA: NIPO TAYARI KUIMBA TAARAB


Baada ya kuachia ngoma yake mpya ‘Sawa’ iliyo tayarishwa na Shirko na kufanya vizuri katika chati za redio mbalimbali, na ngoma hiyo ilikuwa kazi ya kwanza kutoka chini ya label yake, SK Musik.

Msanii wa Kike wa muziki wa Bongo Flava, Sara ‘Shaa’ Kaisi, amesema kuwa yupo tayari kuimba wimbo wa Taarab endapo atapata...
mtunzi mzuri wa ‘Shairi’.

Akiongea kupitia kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Shaa amedai kuwa yeye anaweza kufanya muziki wa aina yoyote hata wa kumtukuza Mungu yaani Injiri.
“Umeniuliza kipindi ambacho ndio nawasiliana na mtu hapa kuhusu hilo, naweza kufanya nikipata Wimbo mzuri, Mtunzi mzuri naimba taarab bila tatizo lolote” Alisema Shaa.
Katika hatua nyingine Msanii huyo amewakaribisha watunzi wa Mashairi ya Taarab kumuandalia wimbo wowote ambao unaweza kuendana nae na kuingia kwenye anga la muziki huo wa Mwambao.

0 comments:

Post a Comment