Pages

Subscribe:

Thursday, November 24, 2016

MWANA FA: SINA HAJA YA KUDANDIA DANDIA TREND ZA SINGELI

Instagram photo by Falsafa_The Choirmaster_BNHrBZJ - JPG
Baada ya kufanya vizuri na ngoma ya ‘Asanteni kwa Kuja”, Mwana FA ameachia ngoma yake mpya, ‘Dume Suruali’ aliyomshirikisha Vee Money. Producer ni Daxo Chali.

Ngoma hiyo ya Mwana FA imeonesha kupokelewa vizuri na mpaka sasa inazidi kufanya vizuri, pongezi kwake, Mbali na hilo, Rapa Mkongwe Hamis ‘Mwana FA’ Mwin’juma, amefunguka na kusema kuwa ana amini aina ya muziki anaoufanya haoni sababu ya kudandia dandia aina ya miziki inayo...
‘Trend’ kwa sasa ikiwemo Singeli. 

Akiongea kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times Fm jana, FA amedai hana mamlaka ya kumkataza msanii yeyote kufanya aina ya muziki anayoitaka lakini kwa yeye hatoweza kufanya Singeli.
“Kama mtu ameamua kurap juu ya mdundo wa Singeli mi ni nani hadi nimkataze? Kulikuwa na kipindi kila anayerap anataka kuimba, sioVmbaya kwenda na Trend, mimi sifikirii kufanya Singeli nauamini sana mziki wangu” Alisema FA. Katika hatua nyingine rapa huyo amedai wimbo wake mpya wa ‘Dume Suruali’ ni muendelezo wa ‘Bado nipo nipo’ kwani yule bachela asiyetaka kuoa ameoa lakini hataki kuonga.

0 comments:

Post a Comment