Pages

Subscribe:

Saturday, November 26, 2016

ALIKIBA ATOA USHAURI KWA WASANII WAKONGWE KWENYE BONGO FLAVA


Huwezi kuwataja wakongwe wa muziki wa Bongo Fleva ukaacha kumtaja mkali wa sauti, hitmaker wa ngoma kama Cinderela. Mackmuga na nyingine kibao ambazo zilitesa kinoma noma kipindi cha nyuma. Najua umeshanielewa kama namzungumzia Alikiba.

Kwasababu ni mmoja kati ya wakali ambao walifanya poa sana miaka ya nyuma na still hadi leo wanafanya poa katika game ya music. Ni wengi sana ambao walipata nafasi kama aliokuwa nayo Alikiba kipindi hicho lakini...
leo hii hawapo tena kwenye ramani ya game ya music.

Alikiba amebonga na kutoa maneno kuntu ambayo kwa maana nzuri inaweza kutumika kama funzo kwa wakongwe hao wa Bongo Fleva.

“Me naomba kuwaambia tu kwamba wajitambue kama muziki umechange, me ni fan wa Bongo Fleva, natamani sana kuwaona wale wakongwe wa Bongo Fleva wawepo hadi leo na wawe wanaendelea kufanya muziki mzuri, ukiangalia wao wameutoa huu muziki mbali sana, hicho ni kitu ambacho sisi tunatakiwa kuwashukuru sana.”

0 comments:

Post a Comment