Pages

Subscribe:

Sunday, April 2, 2017

BARAKAH THE PRINCE: UONGOZI ULIKATAA KUMTUMIA NAJ KWENYE NISAMEHE



Msichana ambaye alitakiwa kuonekana kwenye video ya wimbo wa Barakah The Prince ‘Nisamehe’ aliomshirikisha Alikiba, ni Naj. Hata hivyo chaguo hilo la Barakah pamoja na muongozaji, Meji Alabi kumweka mpenzi wake kama mrembo wa video hiyo lilitoshwa na uongozi wake wa Rockstar4000.

“Hiyo video ilikuwa nishoot na Najma, sema uongozi wangu haukutaka awepo Najma kwenye video,” Barakah alikiambia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir.
“Na director wa video ambaye ni Meji, choice yake ilikuwa ni...
Najma. 

Kwahiyo kilichotokea pale ikabidi atafute msichana ambaye anafanana na Najma, kwahiyo director ndio alimtafuta huyo dada, mimi nilimkuta tu tayari yupo location, tukafahamiana na kufanya hiyo kazi” aliongeza muimbaji huyo.
Kwa sasa Barakah ameachia kazi mpya iitwayo Acha Niende.

0 comments:

Post a Comment