Pages

Subscribe:

Wednesday, April 5, 2017

EDU BOY AJIBU DONGO ALILOPIGWA NA NIKKI MBISHI

Msanii wa Hip Hop anayewakilisha Mwanza, Edu Boy  amefunguka baada ya kufyatuliwa risasi na Rapper mwenzake, Nikki Mbishi kwa kuandika ujumbe ambao Edu Boy ameonesha hajapendezewa nao ujumbe huo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nikki Mbishi aliandika ” Huyu Edo Boy huwa ananiangusha sana kwenye interviews zake sijui ndo utoto! Hebu ngoja...
nikalale zangu.”
(Nikki Mbishi tweet)
Tweet hiyo ilipelekea kuwepo na mjadala mkubwa na watu wengi waliweza kutoa yao ya moyoni huku wengine wakiwa upande wa Edu Boy na wengine upande wa Nikki.
(Edu Boy & Nikki Mbishi Reply Tweet)
Akiongea Jumatano hii, Edu Boy amedai “Kuhusu Nikki Mbishi kwanza kabisa ni mbishi kwa hiyo haina haja ya kuongelea sana, ametweet katika twitter yake anasema kwamba Edu Boy ananiangusha katika Interview, sijui ndio utoto? sasa sijajua kwa nini ananitafuta kwa kuniita mimi mtoto, au labda kuna utoto ndani yangu. Alafu aelewe kabisa sifanyi interview zangu ili kumfurahisha Nikki Mbish. Mbishi si chochote katika muziki wangu, hayupo kabisa katika  akili yangu wala line yangu kwa hiyo akiongea kama namuangusha mimi namuona kama mtu mwingine.

Aliendelea “Mimi kama mimi nafanya Interview juu ya muziki mzuri na wanaomfuatilia Edu Boy wajue Edu Boy yuko wapi? na anafanya nini, anajihusisha na nini sasa hivi, au anakitu gani hapa mjini, Sifanyi Interview ili kumfurahisha Nikki Mbishi, kama hivo anavyosema huyu dogo asipoangalia anaweza asifike mbali, atagombana na kila mtu.

“Ntagombana na kila mtu kivipi sasa? alihoji Edu Boy. “Wimbo wangu wa Naiee nimeongelea wasanii ambao walishanizingua, sijaongelea katika bifu wala sijam-diss  mtu yoyote, ni wimbo ambao nimetoa maelezo.  Anataka kwenye Interview niwe naongelee mimea au wanyama ili kumfurahisha yeye? kitu ambacho hakiwezekani”. Aliongeza msanii huyo.

0 comments:

Post a Comment