Pages

Subscribe:

Friday, April 7, 2017

DIAMOND ATOA WOSIA HUU KWA WATOTO ZAKE


Huwezi kutaja wasanii ambao wamechangia kupeperusha bendera ya muziki wa kizazi kipya duniani bila kutaja jina la ‘Nassib Abdul’ maarufu kama Diamond Platnumz.

Anyway, tukiachana na hilo.. Diamond Platnumz si mgeni kwenye jumbe tata kwenye mitandao ya kijamii. Lakini ujumbe wake mpya kwa watoto wake, Tiffah na Nillan umesababisha...
mjadala mkubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond aliandika.. “Prince & Princess Lion!!!.. Midomo mkaitumie vizuri hiyo watoto…. @princenillan @princess_tiffah”

Haijafahamika kwanini Diamond, ametoa wosia wa namna hiyo na huenda amefanya hivyo kutokana utamaduni wetu sisi Waafrika kupenda kuongea ongea. Pia inawezekana kuwa Diamond  ametumia ujumbe huo kuwaumbua mahasimu wake ambao wamekuwa wakisema kuwa Nillan si mwanaye.
(Instagram post)
Maneno: “Midomo mkaitumie vizuri hiyo watoto” ndiyo yaliyo sababisha povu la haja.

0 comments:

Post a Comment